Magavana wa North Rift waapa kudumisha amani

Tom Mathinji
1 Min Read

Magavana kutoka eneo la North Rift wameapa kuimarisha ushirikiano wao kupitia miradi ya kudumisha amani kwa manufaa ya maendeleo katika maeneo ya mashinani.

Akiongea wakati wa siku ya kwanza ya kongamano la amani la muungano wa kiuchumi wa kaunti za eneo la North Rift,gavana wa George Natembeya alisema juhudi maksus zinatekelezwa kudumisha amani na utangamano.

Natembeya alitumai kuwa mbinu hizo mpya za kudumisha umoja zitafanikiwa na kusitisha uhasama wa kila mara hasa katika maeneo ya mpaka kati ya kaunti hizo nane za North Rift.

Alisema kushughulikiwa kwa maswala kama yale ya mabadiliko ya hali ya hewa kutachangia pakubwa katika kupunguza mizozo.

Gavana wa Pokot magharibi Simon Kachapin alitumai kwamba viongozi wa kaunti za Trans Nzoia, Pokot magharibi , Turkana, Uasin Gishu, Nandi na Elgeyo Marakwet watashirikiana kusitisha uhasama wa kijamii.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *