Maelfu waandamana nchini Australia kundi la waliotengwa

Dismas Otuke
1 Min Read

Maelfu ya raia nchini Australia wameandamana kwenye miji kadhaa nchini humo mapema Jumapili kuunga mkono kundi la watu wa kiasilia waliosahaulika wakitaka kuandaliwe kura ya maoni baadae mwaka huu ya kubadilisha katiba ili watu hao watambulike.

Kampeini hiyo maarufu kama Yes23 ni mojawapo ya mikakati ya mikutano ya hadhara inayounga mabadiliko ya katiba.

Pendekezo la kutambuliwa kwa kundi hili la watu litajumuishwa kwenye kura ya maoni inaotazamiwa kuandaliwa kati ya mwezi Oktoba na Disemba mwaka huu.

Chama kinachoongozwa na Waziri mkuu Anthony Albanese kinaunga mkono mabadiliko ya katiba huku upinzani ukipinga.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *