Ahmed Mohamed Islam almaarufu Modobe amachaguliwa kwa muhula wa tatu kuingoza Jubaland licha ya vikwazo kutoka kwa Somalia, iliyopinga kuchaguliwa kwake kwa muhula wa tatu ikisema amepitisha muda wa kuhudumu uliowekwa.
Madobe alipata uungwaji mkono na wabunge 55 dhidi ya wapinzani wake Faisal Mohamed Matan, aliyeambulia kura 16 na Abubakar Abdi Hassan aliyepata kura 4.
Uchaguzi huo ulikumbwa na mhemuko na ushindani mkali husan wakati wa kampeini huku Waziri Mkuu wa Somalia Hamza Abdi Barre akipinga kuchaguliwa tena kwa Madobe .