Madereva wa malori ya masafa marefu wahofia usalama wao

Tom Mathinji
1 Min Read

Madereva wa malori ya masafa marefu, wameelezea wasiwasi wao kuhusiana na kuongezeka kwa visa vya ukosefu wa usalama katika barabara kuu za Kisumu – Busia na Eldoret – Malaba, ambako madereva huporwa.

Wakiongea Jumatatu mjini Malaba, madereva hao wakiongozwa na mwenyekiti wao, Peter Tanui, walidokeza kuwa majambazi hao wamekuwa wakitumiwa msongamano wa magari  ambao umedumu kwa muda wa wiki mbili kupora bidhaa  zinazosafirishwa.

Tanui sasa anamtaka waziri mpya wa barabara na uchukuzi kuzuru vituo vya mpakani vya  Busia na  Malaba na kushughulikia hali hilo .

Matamshi ya Tanui yaliungwa mkono na dereva mwenzake Hosen Adan, aliyesema kuwa  wametoa makataa ya siku 14 kwa halmashauri ya ukusanyaji ushuru nchini Kenya- KRA, halmashauri ya ukusanyaji ushuru nchini Uganda  – URA  pamoja na ile ya Sudan Kusini kushughulikia swala hilo, la sio hivyo watasitisha uchukuzi wa bidhaa kuelekea Sudan Kusini.

Mmoja wa madereva hao alielezea  jinsi alivyoporwa dola  50,000 za marekani na watu wanaoshukiwa kuwa wanajeshi wa Sudan Kusini.

Msongamano huo wa malori hayo ya masafa marefu, umefika Kanduyi, huku madereva hao wakihofia huenda ukafika Webuye.

TAGGED:
Share This Article