Madereva wa Kenya kujituma dhidi ya mibabe, mashindano ya WRC

Dismas Otuke
2 Min Read

Mashindano ya magari ya WRC Safari Rally yanaandaliwa kati ya Machi 28 na 31 huku yakiwashirikisha madereva 29.

Hata hivyo, hakuna dereva wa Kenya atakayeshiriki kitengo kikuu cha Rally 1.

Baadhi ya madereva mashuhuri watakaoshiriki ni wale wa kampuni ya Toyota Gazoo kama vile:-Ellyfin Evans wa Uingereza, Katsuta Takamoto wa Japani na Kalle Rovanpera kutoka Finland.

Madereva wa kampuni ya magari ya Hyundai ni pamoja na:-Thierry Neuville kutoka Ubelgiji, Ott Tanak wa Estonia na Esapeka Lappi wa Finland.

Timu ya tatu ya magari ni M-Sport Ford ikiwa na:- Grégoire MUNSTER Luxenmborg, Jourdan SERDERIDIS wa Ugiriki na Adrien FOURMAUX kutoka Ufaransa.

Madereva wa haiba ya juu wa Kenya wanashiriki kitengo cha Rally 2 akiwemo bingwa mara tano wa Safari Rally Carl Tundo akisaidiwa na Tim Jessop wakiendesha gari la Ford Fiesta na bingwa wa Afrika Karan Patel akishirikiana na Tausiff Khan wakiwa na gari la Skoda Fabia.

Wengine ni Samman Vohra wakishirikiana na Alfir Khan kwa gari la Skoda Fabia Evolution na Aakif Viran akiwa na mwelekezi wake Zahir Shah wakiendesha gari la Skoda Fabia.

Hamza Anwar akishirikiana na Adnin Din ndiye mshiriki pekee katika kutengo cha Rally 3, huku waliosalia wakiwa ni pamoja na Nikhil Sachania, Minesh Rathod na Andrew Muiruri.

Share This Article