Madaktari wasimama kidete, wakataa ofa ya serikali na kuapa kuendelea kugoma

Dismas Otuke
1 Min Read

Chama cha madaktari nchini, KMPDU kimeapa kuendelea na mgomo wao ambao uliingia wiki ya tatu siku ya Jumatatu.

Kulingana na Katibu mKuu wa KMPDU Dkt. Davji Atellah, watasitisha mgomo iwapo tu serikali itatekeleza kikamilifu mkataba wa maelewano wa mwaka 2017-2021.

Haya yanajiri muda mfupi baada ya seikali kutangaza Jumanne kuwa itatekeleza nyongeza hiyo na kuwaajiri madaktari wanagenzi na kuwataka wasitishe mgomo huo ambao umeingia wiki ya tatu.

Sekta ya afya ya umma imesambaratishwa na mgomo huo wa madaktari na hali imekuwa mbaya zaidi, baada ya wataalam wa maabara kutangaza kuanza mgomo wao Jumatano, Aprili 3.

TAGGED:
Share This Article