Madaktari wahitimisha mgomo

Marion Bosire
1 Min Read

Viongozi wa muungano wa madaktari nchini KMPDU wametia saini mkataba wa kurejea kazini na mwajiri wao ambaye ni serikali kupitia kwa wizara ya afya.

Hatua hii inahitimisha mgomo wa wahudumu hao wa sekta ya afya uliodumu siku 56.

Jana Jumanne Mei 7, 2024 maafisa wa chama cha KMPDU walisema hawakuwa tayari kutii agizo la mahakama ya masuala ya ajira la kuafikia makubaliano katika muda wa saa 48.

Haya yanajiri saa chache tu baada ya muungano wa upinzani Azimio la Umoja One Kenya kutoa makataa ya siku mbili kwa serikali kumaliza mgomo huo wa madaktari.

Share This Article