Madaktari wa Kiambu wasitisha mgomo wa miezi mitano

Dismas Otuke
1 Min Read

Madaktari wa kaunti ya Kiambu wametangaza kusitisha mgomo uliodumu kwa miezi mitano sasa baada ya kuafikiana .

Katibu Mkuu wa chama cha matabibu na wataalam wa meno (KMPDU) Devji Atella ametangaza kuwa wamemaliza mgomo baada ya kuafikiana kuhusu matakwa yao na serikali ya kaunti ya Kiambu.

Mgomo huo ukiwa umedumu kwa takriban siku 150 Na ulikuwa umedumaza huduma za matibabu katika hospitali zote za kaunti hiyo.

Madaktari hao wamesaini mwafaka wa kurejea kazini Kati ya maafisa wa KMPDU na Gavana wa kaunti ya Kiambu Kimani wa Matangi.

Website |  + posts
Share This Article