Madai dhidi ya Jaji Mohammed Noor Kullow yatupiliwa mbali

Martin Mwanje
1 Min Read
Jaji wa Mahakama ya Rufaa Patrick Kiage akimkabidhi Rais William Ruto ripoti ya uchunguzi wake

Jopo lililoteuliwa na Rais William Ruto kuchunguza madai dhidi ya Jaji wa Mahakama ya Mazingira na Ardhi Mohammed Noor Kullow limependekeza kurejeshwa kwa jaji huyo kazini. 

Hii ni baada ya jopo hilo lililoongozwa na Jaji wa Mahakama ya Rufaa Patrick Kiage kutupilia madai yote aliyolimbikizwa Jaji Kullow.

 

Madai hayo yalijumuisha Jaji Kullow kuchelewa kutoa uamuzi na hukumu katika kesi alizosikiliza, kukosa kutoa sababu za kuchelewa huko, kukosa kujibu barua za Jaji Mkuu, kusalia na faili ya mahakama na hivyo kunyima upande mmoja katika kesi haki ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi, kutoa uamuzi na hukumu bila kutoa notisi na utepetevu kazini.

Jopo lililoongozwa na Jaji Kiage lilimkabidhi Rais Ruto ripoti yake katika hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Nairobi leo Jumatatu asubuhi na kuhudhuriwa na miongoni mwa wengine, Mwanasheria Mkuu Dorcas Oduor.

Kufuatia matokeo ya jopo hilo, Rais Ruto anatarajiwa kutoa agizo la Jaji Kullow kurejea kazini.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *