Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu amesisitiza kwamba utekelezaji wa mtaala wa umilisi CBC unaendelea kwa njia iliyo sawa.
Akizungumza mbele ya bunge la Seneti, Machogu alikiri uwepo wa changamoto hasa za miundomsingi ambazo zinashughulikiwa hatua kwa hatua.
Machogu alifichua kwamba wizara yake inaendelea kuwasiliana na benki ya dunia ili kupata ufhadili wa kujenga vituo 1867 vya masomo na vitu vingine vinavyohitajika kwa gharama ya shilingi bilioni 3.36.
Waziri aliwataka wabunge wasaidie pia kwa kujenga vituo kama hivyo kupitia kwa hazina ya ustawi wa maeneo bunge.
Alisema serikali imesambaza pesa za kufadhili elimu katika sekondari msingi kote nchini ambapo kila mwanafunzi amelipiwa kati ya shilingi elfu 15 na elfu 40.
Walimu 38,917 alisema wameajiriwa kufikia sasa huku kukiwa na mipango ya kuajiri wengine elfu 20 baadaye mwaka huu.
Shule zote zimepatiwa vitabu vya kiada vya gredi ya 7.