Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu anatarajiwa kufika mbele ya kamati ya bunge kuhusu elimu kutoa ufafanuzi kuhusu utata uliopo katika mfumo mpya wa kuwafadhili wanafunzi vyuoni.
Wabunge wamehofia kuwa huenda mfumo huo mpya wa ufadhili ukawafungia nje wanafunzi wengi kutokana ucheleweshaji wa kutolewa kwa hela ambao unaletwa na mchakato uliowekwa kabla ya wanafunzi kupokea pesa hizo, hali ambayo itachangia wengi wa wanafunzi walioratibiwa kujiunga na vyuo kuanzia wiki ijayo kuchelewa kuripoti.
Wabunge wanataka mfumo wa zamani wa kufadhili masomo vyuoni ambapo wanafunzi wengi walikuwa wakilipa karo ya shilingi 16,000 kwa mwaka kwa masomo ya shahada.
Kulingana na Afisa Mkuu Mtendaji wa Bodi ya Kutoa Mikopo kwa Wanafunzi, HELB Charles Ringera, ni wanafunzi 75,000 waliokuwa wametuma maombi ya mikopo ya masomo kufikia jana Jumatano.