Machogu asikitishwa na idadi kubwa ya wanafunzi waliopata alama ya E

Tom Mathinji
1 Min Read

Waziri wa elimu, Ezekiel Machogu ameagiza uchunguzi ufanywe kuhusu matokeo duni ya zaidi ya watahiniwa 48,000 katika mtihani wa KCSE mwaka 2023.

Akiongea katika shule ya upili ya wasichana ya Moi girls mjini Eldoret wakati wa kutangaza matokeo hayo siku ya Jumatatu, Machogu hata hivyo alisema matokeo ya mwaka 2023 ya mtihani huo yamekuwa bora kuliko yale ya mwaka 2022.

Alielezea wasiwasi wake kuhusu idadi kubwa ya watahiniwa waliopata alama ya E, na kutaka uchunguzi ufanywe mara moja kuhusu suala hilo, na ripoti iwasilishwe afisini mwake katika kipindi cha mwezi mmoja.

Machogu alisema watahiniwa katika masomo 14 yakiwemo kiingereza na historia hawakunakili matokeo mazuri.

Aidha, waziri huyo alisema matokeo hayo yalitokana na hatua zilizochukuliwa kuzuia udanganyifu wa mitihani.

Share This Article