Serikali imetenga siku ya kutekelezwa kwa hatua za kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi pamoja na upanzi wa miche bilioni 15 kufika mwaka 2032.
Katibu katika wizara ya usalama wa taifa Dkt. Raymond Omollo, atazindua siku hii Novemba 4,2024 katika eneo chepechepe la Ondiri kaunti ya Kiambu.
Mpango huo ambao unalenga kuongeza utandu wa misitu kutoka asilimia 12 hadi asilimia 30.
Kulingana na wizara ya usalama wa taifa, mpango huo utaongozwa na machifu na utakuwa ukitekelezwa katika kila kata, ijumaa ya kwanza ya kila mwezi..
Kupitia mpango huu, kila kata litajizatiti kupanda miche 250 siku hiyo, ili kufanikisha kuimarisha mazingira bora hapa nchini.
Zoezi hili la kila mwezi, linahakikisha Kenya inaafikia malengo yake kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi.
Kila mwezi Machifu watashirikiana na jamii katika upanzi wa miti na utoaji mafunzo kuhusu utunzi wa mazingira.