Mabingwa watetezi Senegal warushwa kundi moja na Cameroon michuano ya AFCON 2023

Dismas Otuke
2 Min Read

Mabingwa watetezi Senegal ukipenda Teranga Lions wamejumuishwa kundi C pamoja na Cameroon katika makala ya 34 ya kipute cha kuwania kombe la mataifa ya Afrika, AFCON kitakachoandaliwa nchini Ivory Coast kati ya Januari 13 na Februari 11 mwakani.

Timu nyingine kundini humo ni Guinea na Gambia.

Wenyeji The Elephants ya Ivory Coast watafungua dimba dhidi ya Guinea Bissau huku mataifa mengine kundini A yakiwa Super Eagles ya Nigeria na Equitorial Guinea.

Mabingwa mara saba Misri ukipenda The Pharaohs, watapambana na mabingwa mara nne Black Stars kutoka Ghana, visiwa vya Cape Verde na Musumbiji.

Makundi

Group A: Ivory Coast, Nigeria, Equatorial Guinea, Guinea Bissau

Group B: Egypt, Ghana, Cape Verde Islands, Mozambique

Group C: Senegal, Cameroon, Guinea, Gambia

Group D: Algeria, Burkina Faso, Mauritania, Angola

Group E: Tunisia, Mali, South Africa, Namibia

Group F: Morocco, DR Congo, Zambia, Tanzania

Desert Foxes ya Algeria itapimana nguvu na Burkina Faso, Mauritania na Palancas Negras kutoka Angola katika kundi D wakati kundi E likisheheni Tunisia almaarufu the Carthage Eagles, Afrika Kusini na Brave Warriors ya Namibia.

Atlas Lions ya Morocco imo kundi la mwisho la F pamoja na Jamhuriya Demokrasia ya Congo, Chiplolopolo ya Zambia na Taifa Stars ya Tanzania.

Droo hiyo iliandaliwa jana Alhamisi usiku mjini Abdijan, Ivory Coast na kuongozwa na kinara wa CAF Dkt. Patrice Motsepe.

Share This Article