Mabingwa wa OIimpiki Faith Kipyegon na Beatrice Chebet, waanatarajiwa kuwasili nchini Jumanne usiku kutoka Paris Ufaransa.
Kipyegon alihifadhi taji ya mita 1,500 ikiwa mara yake ta tatu kushinda dhahabu hiyo ya Olimpiki na kushinda pia nishani ya fedha katika mita 5,000.
Chebet naye alishinda dhahabu katika mita 5,000 na mita 10,000 akiwa mwanamke wa kwanza wa Kenya kutwaa dhahabu ya Olimpiki katika mita 10,000.
Wanariadha hao watalakiwa katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta na Waziri wa Michezo Kipchumba Murkomen.
Mshindi mwingine wa nishani ya dhahabu katika mita 800 Emmanuel wa Wanyonyi anatarajiwa kuwasili nchini Jumatano Alfajiri.
Kenya ilimaliza ya 17 katika michezo ya Olimpiki kwa dhahabu 4 fedha 2 na shaba 5.