Fainali za 34 za kuwania kombe la mataifa ya Afrika zitaanza rasmi nchini Ivory Coast Jumamosi ,Januari 13 na kukamilika Februari 11.
Misri The Pharoes ndio timu iliyofanikiwa zaidi ikitwaa mataji 7, miaka ya 1957, 1959, 1986, 1998, 2006, 2008 na 2010.
Cameroon ukipenda Indomitable Lions wamenyakua mataji matano miaka 1984, 1988, 2000, 2002 na 2017 wakifuatwa na Black Stars ya Ghana walio na Ghana walio na mataji manne miaka ya 1963, 1965, 1978 na 1982.
Super Eagles ya Nigeria wameibuka mabingwa mara tatu;1980, 1994 na 2013 huku Algeria ,Ivory Coast na Jamhuri ya Demokrasia ya Congo wakishinda mataji mawili kila moja.
Mataifa manane ya Senegal,Tunisia,Zambia,Sudan,Congo,Ethiopia,Afrika Kusini na Morocco yamenyakua kombe la AFCON mara moja kila moja.