Mabanati wa Kenya wapigwa laza nyumbani na Cameroon

Junior Starlets walifuzu kwa Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza mwaka jana katika Jamhuri ya Dominika.

Dismas Otuke
1 Min Read

Ndoto ya timu ya taifa ya Kenya kwa wasichana wasiozidi umri wa miaka 17, kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya pili mwaka huu, imefifia baada ya kulazwa bao moja kwa bila na Cameroon katika mkumbo wa kwanza wa raundi ya tatu uliochezwa ugani Nyayo Jumapili jioni.

Wageni walipachika bao pekee na la ushindi kunako dakika ya 25 kupitia kwa nahodha Tiwa Melong Lys kwa njia ya kichwa .

Kenya ni sharti sasa washinde mkumbo wa pili mabao 2-0 Aprili 25, ili kufuzu kwa Kombe la Dunia.

Junior Starlets walifuzu kwa Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza mwaka jana katika Jamhuri ya Dominika.

Fainali za tisa za Kombe la Dunia zitaandaliwa barani Afrika kwa mara ya kwanza nchini Morocco, kati ya Oktoba 17 na Novemba 8 mwaka huu.

 

 

Website |  + posts
Share This Article