Timu ya Kenya kwa wasichana walio chini ya umri wa miaka 17,imeimarisha mazoezi yake leo katika uwanja wa Kasarani, kujiandaa kwa mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia.
Junior Starlets wanaofunzwa na kocha Mildred Cheche, wanajitayarisha kuwaalika Uganda Jumamosi hii katika raundi ya pili mkondo wa kwanza kufuzu kwa Kombe la Dunia.
Kenya ilifuzu kwa raundi ya pili baada ya kuibandua Namibia, kwenye raundi ya kwanza huku Uganda wakiwatema nje Zimbabwe, katika mechi nyingine ya raundi ya kwanza.
Starlets wanawinda kufuzu Kwa Kombe la Dunia mwaka huu mwa mara ya pili baada ya kushiriki mwaka 2024, katika Jamhuri ya Dominica.