Halmashauri ya Utalli Kenya, yamtuza Sawe

Dismas Otuke
1 Min Read

Halmashauri ya Utalii Kenya (KTB), imemtuza mshilikizi wa rekodi ya dunia ya Marathon Sabastian Sawe, siku nne za matembezi na kujivinjari popote nchini.

KTB imesema kama njia ya kumsherehekea Sawe, kufuatia ushindi wake wa London marathon na kuandikisha rekodi mpya ya dunia  ya saa 1 dakika 59 na sekunde 30,itamwalika kujivinjari kwa siku nne eneo lolote alitakalo humu nchini.

Afisa Mkuu mtendaji wa KTB, June Chepkemei, amesema ziara hiyo maarufu kama Champion’s Retreat, itamwezesha Sawe kupumzika baada ya kazi ngumu.

Share This Article