Maandamano yaendelea DRC kupinga matokeo ya kura za Urais

Dismas Otuke
1 Min Read

Maafisa wa polisi katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo waliendelea na makabiliano na wafuasi wa upinzani wanaotaka kufutiliwa na kurejelewa kwa kura za urais kufuatia madai ya wizi wa kura za wiki iliyopita.

Maafisa wa tume ya uchaguzi hawajafichua idadi ya vituo vya kupiga kura vilivyofunguliwa siku ya uchaguzi Disemba mwezi huu .

Inakisiwa kuwa takriban vituo 75,000 vilifunguliwa huku ikikisiwa kuwa wapiga kura milioni 44 walishiriki uchaguzi huo.

Matokeo ya awali yanaashiria kuwa Rais Felix Tshisekedi ameshinda muhula wa pili akiwa amezoa asilimia 80 ya kura 80 zote.

Share This Article