Maandalizi ya Siku ya Mashujaa

Martin Mwanje
1 Min Read

Pilikapilika za kuandaa Siku ya Mashujaa zimeshika kasi katika kaunti ya Kericho.

Kaunti hiyo sasa imegeuka kuwa mwenyeji wa viongozi wa ngazi za juu serikalini wanaofika kujionea maandalizi ya siku hiyo.

Siku ya Mashujaa itaadhimishwa katika uwanja Kericho Green Gardens Ijumaa wiki hii, Oktoba 20, 2023.

Naibu Rais Rigathi Gachagua leo Jumatatu aliwaongoza viongozi wengine wakiwemo Mawaziri Florence Bore wa Leba na Susan Nakhumicha wa Afya kuangazia hatua zilizopigwa na kaunti hiyo kufanikisha maadhimisho ya siku hiyo.

Wote hao walilakiwa na Gavana wa kaunti hiyo Erick Mutai aliyewahakikishia kuwa maandalizi ya hafla hiyo yanaendelea vizuri.

Kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ya Siku ya Mashujaa ni “Upatikanaji wa Afya kwa Wote”.

Rais Ruto ataliongoza taifa katika kusherehekea siku hiyo Ijumaa wiki hii.

 

 

Share This Article