Maandalizi ya mazishi ya marehemu Francis Ogolla yaanza

Tom Mathinji
1 Min Read
Mkuu wa vikosi vya ulinzi marahemu Jenarali Francis Ogolla.

Kufuatia ajali ya helikopta ilisababisha kifo cha mkuu wa vikosi vya ulinzi Jenerali Francis Ogolla, wizara ya ulinzi imetoa ratiba ya shughuli zitakazofanyika kabla ya mazishi yake.

Taarifa ya vikosi vya ulinzi hapa nchini KDF, ilisema Marehamu Jenerali Ogolla atazikwa kuambatana na kanuni za kijeshi na kuambatana na matakwa yake.

Kutakuwa na hafla ya heshima za kijeshi na ibada ya wafu itakayoandaliwa katika uwanja wa michezo wa kijeshi wa Ulinzi Complex huko Lang’ata, katika kaunti ya Nairobi kuanzia saa saba mchana leo.

Rais William Ruto ataongoza shughuli ya heshima za kijeshi na baadaye kuhudhuria ibada ya wafu katika kaunti ya Nairobi, na hafla ya mazishi kesho huko Siaya. Wizara ya ulinzi imewaomba waombolezaji watakaohudhuria mazishi ya mwendazake kuwa wamekaa itimiapo saa tano asubuhi.

Ibada ya mazishi itaogozwa na kanisa katika uwanja wa  shule ya msingi ya Senator Obama K’Ogello katika kijiji cha  Ng’iya.  Baadaye jenerali Ogolla atazikwa kijijini humo, kaunti ndogo ya Alego Usonga kaunti ya Siaya.

Ijumaa ya terehe 26 kutakuwa na misa ya wafu katika uwanja wa michezo wa kijeshi Ulinzi Complex jijini Nairobi. Familia ya marehemu imesema mazishi ya Jenerali Ogolla yameharakishwa kuambatana na maagizo yake kwamba atakapoaga azikwe katika muda wa saa 72.

Share This Article