Maafisa watatu wa polisi na raia mmoja wameshtakiwa katika mahakama moja ya Kericho kwa wizi wa kimabavu.
Wanne hao Kipyegon Ngetich, Chamdany Kipkirui, Robert Ngetich na Kipngetich Rono, walikanusha mashtaka hayo mbele ya hakimu mkuu mwandamizi Johnson Monguti.
Wanadaiwa kuwa tarehe mwezi Disemba 28, 2023, katika mtaa wa Upper Hill kaunti ndogo ya Bureti, kaunti ya Kericho, wakiwa pamoja na wengine ambao hawako mahakamani walimuibia Wesley Kipngeno gari lake wakiwa wamejihami na bastola.
Gari hilo KDE 005K la thamani ya shilingi 1,520,000, lilikuwa na shilingi 150,000 ndani yake wakati wa wizi huo wa kimabavu.
Washukiwa hao waliachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni mbili kila mmoja. Walishindwa kupata dhamana hiyo na sasa wanazuiwa katika kituo cha polisi cha Litein.
Kesi hiyo itatajwa Aprili 10, 2024.