Maafisa wakuu wa Huduma ya Taifa ya Polisi wahamishwa

Tom Mathinji
1 Min Read
Maafisa wakuu wa huduma ya taifa ya polisi wahamishwa.

Maafisa wa ngazi za juu wa Huduma ya Taifa ya Polisi wamehamishwa, katika mabadiliko yaliyotangazwa na Inspekta Jenerali wa polisi Douglas Kanja.

Katika mabadiliko hayo ya siku ya Alhamisi, kamanda wa polisi kaunti ya Kiambu Michael Muchiri, ameteuliwa kuwa msemaji wa polisi na kuchukua mahala pa Dkt. Resila Onyango ambaye ametajwa kuwa kamanda wa kitengo cha polisi kinachoshughulikia maswala ya diplomasia.

Maafisa wengine waliohamishwa ni pamoja na kamanda wa kaunti ya Nairobi Adamson Bungei, ambaye ameteuliwa kuwa mkurugenzi wa operesheni katika makao makuu ya polisi, wadhifa ulioshikiliwa na George Sedah ambaye sasa amehamishwa kaunti ya Nairobi.

Kamanda wa polisi kaunti ya Kwale Ali Nuno amepandishwa cheo na kuwa kamanda wa polisi eneo la Pwani, huku  Dkt.. Mwangi Wanderi akiteuliwa mkurugenzi wa maswala ya wafanyakazi katika makao makuu ya polisi.

Daniel Korir  sasa ndiye kamanda wa kitengo cha polisi wa angani (KAPU), naye Michael Sang ndiye mkuu wa idara ya uchunguzi wa makosa ya jinai eneo la Mashariki.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *