Maafisa wa usalama watambua makaburi zaidi Shakahola

Martin Mwanje
1 Min Read

Maafisa wa usalama wanaoendeleza shughuli ya kuwasaka wafuasi na manusura wa dhehebu la Good News International linaloongozwa na mhubiri Paul Mackenzie wametambua makaburi mengine 40 ambayo yanakisiwa kuwa na zaidi ya mwili mmoja.

Maiti 12 zilifukuliwa siku ya kwanza katika awamu ya nne ya kufufua miili ya wafuasi wa dhehebu hilo katika maeneo ya Shakahola jana Jumatatu.

Miili hiyo inafikisha 350 idadi ya miili iliyofukuliwa katika msitu wa Shakahola na jumla ya idadi ya walioangamia kufikia 351 hadi kufikia sasa baada ya mtu mmoja kufariki hospitalini.

Shughuli hiyo ilianza jana Jumatatu katika boma la mshukiwa mmoja kwa jina Titus Musyoka ambapo miili mitatu inayoaminika kuwa ya wanawe ilifukuliwa. Musyoka ni mmoja wa washukiwa wa Mackenzi ambaye amezuiliwa na polisi.

Shughuli hiyo itarejelewa leo Jumanne.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *