Maafisa wa usalama wasambaratisha shughuli za magaidi Garissa

Tom Mathinji
1 Min Read

Maafisa wa usalama wamesambaratisha shughuli za kundi la magaidi katika eneo la Ijaara kaunti ya Garisaa, wakati wa operesheni ya kiusalama iliyotekelezwa katika eneo hilo.

Wakati wa operesheni hiyo iliyosababishwa na habari za kijasusi, mitungi ya gesi ya kujitengenezea, na vifaa vya kutengeneza vilipuzi, vilipatikana.

“Mnamo Oktoba 20, 2024, maafisa wa kitengo cha operesheni maalum SOG kutoka eneo la Ijaara, walinasa mitungi ya gesi ya kujitengenezea na vifaa vya kutengeneza vilipuzi,” ilisema huduma ya taifa ya polisi.

Kulingana na taarifa hiyo ya polisi, operesheni ya maafisa hao ilihakikisha eneo hilo ni salama kwa wakazi

“kundi hilo la kutekeleza operesheni maalum litaendelea kutekeleza The SOG continues to play a critical role in protecting the borders of our country against security threats,” NPS assured.

Website |  + posts
Share This Article