Maafisa wa usalama walimuua mwizi mmoja wa mifugo aliyejihami katika eneo la Marigat kaunti ya Baringo siku ya Ijumaa, kufuatia ufiatulianaji risasa mkali.
Polisi walikuwa kwenye gari wakielekea shule ya msingi ya Arabal, kuikarabati baada ya kuporwa ndiposa watu wawili waliojihami kwa bunduki waliposimamisha gari la wanajeshi hao na kukazuka ufyatulianaji wa risasi katika makutano ya barabara ya Embossos.
Mmoja wao aliuawa papo hapo huku mwingine mmoja akipelekwa hospitalini na wanajeshi hao akiwa na majeraha.
Maafisa hao walipata bunduki aina ya AK 47 na risasi kadhaa.
Haya yanajiri katika eneo hilo lenye utovu wa nidhamu siku chache baada ya waziri wa Usalama wa taifa Githure Kindiki, kuzuru maeneo ya Baringo,Samburu na Laikipia kukadiria hali ya usalama.