Kampuni ya Red Cross imewatuma maafisa wake ili kuwaokoa abiria 51, waliokwama ndani ya basi kwenye mafuriko huko Tana River.
Maafisa wa Red Cross wametumia mashua mbili ili kuwaokoa abiria walioonekana ndani ya basi ambalo limezingirwa na maji ya mafuriko.
Abiria hao walikuwa wakisafiri kutoka Garisa kuelekea Nairobi wakati basi hilo lilipozingirwa na maji ya mafuriko katika kijiji cha Tulla kaunti ya Tana River.
Mafuriko hayo yamesababishwa na mvua kubwa inayonyesha katika eneo hilo.