Maafisa wa KEPHIS wanasa mbegu bandia kaunti ya Meru

Tom Mathinji
1 Min Read
Maafisa wa KEPHIS wanasa mahindi bandia kauntinya Meru.

Huku msimu wa upanzi unapokaribia, maafisa wa shirika la ukaguzi wa afya ya mimea KEPHIS kwa ushirikiano na maafisa wa polisi kaunti ya Meru, wamenasa mbegu bandia ya mahindi katika soko la  Mikinduri, kaunti ndogo ya Tigania Mashariki, kaunti ya Meru.

Afisa wa KEPHIS Geoffrey Malembe, alisema walifanya msako katika duka moja kwenye soko hilo, na kumtia nguvuni mfanyabiashara aliyekuwa akipakia na kuuza mbegu hiyo bandia ya mahindi.

Kwa mujibu wa afisa huyo, mbegu zilizoidhinishwa huwekwa dawa ya kuvu, lakini mbegu zilizonaswa zilikuwa tu zimepakwa rangi nyekundu ambayo hutumiwa kwa ujenzi.

Malembe alisema ni wafanyabiashara tu waliodhinishwa na KEPHIS, ndio wanakubaliwa kupakia na kuuza mbegu zilizoidhinishwa.

Kwa upande wake kamishna wa kaunti ya Meru Jacob Ouma, alisema kuna uwezekano mbegu bandia zinauzwa hapa nchini, akiwaonya wakulima kuwa makini zaidi kuhakikisha mbegu wanazonunua ni halali.

TAGGED:
Share This Article