Maafisa wa KDF wamsaidia mama kujifungua kaunti ya Baringo

Tom Mathinji
1 Min Read

Maafisa wa vikosi vya ulinzi nchini, KDF wanaotekeleza operesheni “Maliza Uhalifu” katika eneo la North Rift, walimsaidia mama kujifungua mtoto wakati wa siku ya Jamhuri katika kambi ya wanajeshi ya Mukutani, kaunti ya Baringo.

Mwanamke huyo mjamzito Jenty Lesupen mwenye umri wa miaka 20, anasemekana kuwasili katika kambi hiyo akiwa na maumivu ya kujifungua na kusababisha maafisa hao kuingilia kati ili kumsaidia.

Jenty Lesupen alinifungua mtoto wa kike katika kambi ya jeshi.

Licha ya changamoto zilizopo kutokana na uhaba wa vifaa vya kujifungulia kina mama, matabibu hao wa KDF walifanikisha kujifungua salama kwa mwanamke huyo.

Lesupen alijifungua mtoto wa kike aliyekuwa na uzani wa kilo 5.5.

Punde tu baada ya kujifungua, mama huyo na mtoto wake walipelekwa katika hospitali ya Marigat kwa uchunguzi zaidi wa kimatibabu.

Kata ya Mukutani inakumbwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa kituo cha afya, kwa kuwa kituo kilichokuwapo kilifungwa kutokana na utovu wa usalama.

TAGGED:
Share This Article