Maafisa wa KDF wahusika katika ajali ya ndege

Tom Mathinji
1 Min Read

Maafisa kadhaa wa vikosi vya ulinzi vya Kenya KDF, waliokuwa wakipiga doria katika msitu wa Boni, wanahofiwa kufariki baada ya ndege walimokuwa wakisafiria kuanguka.

Kulingana na taarifa siku ya jumapili, ndege ya hiyo ya helikopta ya jeshi la wanahewa aina ya Huey, ilianguka Jumatatu ilipokuwa ikipiga doria wakati wa usiku.

“Wanajeshi hao walikuwa sehemu ya maafisa wanaoshika doria usiku na mchana katika msitu wa Boni chini ya kauli mbiu  ‘Operation Amani Boni’,” ilisema taarifa hiyo.

Wakati huo huo vikosi vya ulinzi nchini KDF, vinaomboleza na familia ya walioangamia.

Kundi la uchunguzi limetumwa katika eneo la mkasa kubainisha chanzo cha ajali hiyo.

TAGGED:
Share This Article