Maafisa wa idara ya upelelezi wa makosa ya jinai DCI, wanawatafuta washukiwa wa misururu ya ujambazi na mauaji Jijini Nairobi.
Kulingana na idara hiyo kupitia ukurasa wake wa X, visa hivyo vinadaiwa kutekelezwa katika eneo la Embakasi, Nairobi.
“Idara ya DCI inatoa wito kwa wananchi walio na habari kuhusu washukiwa hao kuzitoa ili waweze kutiwa nguvuni,” ilisema idara ya DCI.
Aidha idara hiyo iliwataka washukiwa hao kujisalimisha katika kituo cha polisi kilicho karibu nao, ili hatua zaidi zichukuliwe.
“Habari kuwahusu zinaweza wasilishwa katika kituo cha idara ya DCI Embakasi, katika kituo cha polisi kilicho karibu au kupitia nambazri za #FichuaKwaDCI 0800722203 au 999,911 and 112.