Maafisa wa DCI wanasa washukiwa 41 wa biashara haramu Nairobi

Dismas Otuke
1 Min Read

Maafisa wa ujasusi wa DCI wamenawasa washukiwa 41 walipatikana wakiendesha biashara haramu katika jengo moja ambalo halijakamilika katika barabara ya Lunga kaunti ya Nairobi.

Haya yamejiri huku kukiripotiwa ongezeko la visa vya biashara haramu ikiwemo mafuta ya petroli yaliyochafuliwa na ufyonzaji wa mafuta kutoka kwa magari.

Malori matano ya kubebea mafuta yalipatikana katika eneo la msako huku polisi wakisema kuwa zaidi ya lita 17,000 za dizeli na lita 6,000 za petroli ,jenereta 30 na mabomba ya kufyonza mafuta pamoja na madumu yalinaswa .

Maafisa wa DCI wakiambatana na maafisa kutoka mamlaka ya kudhibiti kawi nchini EPRA walikuwa kwenye eneo la tukio na kutathmini uhalifu huo

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article