Maafisa wa DCI wanasa Pombe bandia Nairobi

Tom Mathinji
1 Min Read
DCI wanasa Pombe bandia.

Maafisa wa polisi wamenasa pombe bandia na mihuri ghushi ya halmashauri ya ukusanyaji ushuru nchini KRA, katika maeneo ya Kahawa Sukari na Kamulu Jijini Nairobi.

Katika operesheni iliyotekelezwa na maafisa wa DCI na wenzao wa halmashauri ya KRA, chupa 1078 za pombe hiyo bandia, lita 630 ya ethanol, mihuri ya KRA, chupa 10,300 ambazo hazikuwa na chochote na vifuniko vya chupa vilipatikana.

Mihuri ya KRA iliyonaswa katika operesheni hiyo.

Kulingana na DCI kupitia mtandao wake wa twitter siku ya Jumamosi, pombe hiyo ni ya thamani ya shilingi 500,000, huku stampu hizo za KRA zikiwa za thamani ya shilingi milioni nne.

Maafisa wa polisi wameanzisha uchunguzi kubaini chanzo cha pombe hiyo bandia na mihuri hiyo ya halmashauri ya KRA.

Share This Article