Maafisa wa DCI wanasa mihadarati katika uwanja wa ndege wa JKIA

Tom Mathinji
1 Min Read

Maafisa wa polisi kutoka kitengo cha DCI wamenasa mihadarati aina ya methamphetamine, katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta.

Kulingana na  DCI, mihadarati hiyo iliyokuwa ikisafirishwa kuelekea Jakarta, Indonesia ilikuwa imefichwa katikati ya bidhaa zingine, zilizotajwa kuwa vifaa vya baisikeli.

Mihadarati hiyo inaaminika kuingizwa humu nchini kutoka Moroni, Comoros.

Operesheni inayoongozwa na maafisa wa polisi wa Kimataifa Interpol, imezinduliwa kuwatambua wanaoendesha biashara hiyo haramu ili wakamatwe na kufunguliwa mashtaka.

DCI  iliapa kuendeleza msako dhidi ya mihadarati huku ikionya kwamba hakuna yeyote atasazwa katika Operesheni hiyo.

“Vita dhidi ya utumizi na biashara ya mihadarati vimeimarishwa hapa nchini na DCi inaonyw kwamba Kenya haina nafasi ya biashara hiyo haramu,” ilisema DCI

TAGGED:
Share This Article