Maafisa wa DCI wanasa gari linalotumiwa kufanya wizi Syokimau

Tom Mathinji
1 Min Read

Maafisa wa Idara ya Upelelezi wa makosa ya Jinai (DCI) wamenasa gari ambalo limekuwa likihusika katika misururu ya wizi katika eneo la Syokimau.

Kulingana na maafisa hao, kukamatwa kwa gari hilo kulitokana na malalamishi  ya wakazi ambapo nyumba zao zilivunjwa wakati wa mchana na mali yao kuibwa.

Video za kamera za usalama, CCTV zilizosambazwa katika mitandao ya kijamii zilinakili gari hilo aina ya Toyota Vanguard.

Wakitekeleza operesheni hiyo, kundi la maafisa wa DCI waliwafumania washukiwa katika eneo la Roasters.

Washukiwa waliokuwa ndani ya gari hilo walikaidi agizo la kusimama na kutorokea eneo la Baba Dogo.

Baadaye waliacha gari hilo katika mtaa wa Ngei na kutoroka kwa miguu.

Ndani ya gari hilo, polisi walipata runinga tano, tarakilishi na nambari za usajili za magari miongoni mwa vifaa vingine.

Polisi wameanzisha msako dhidi ya washukiwa hao waliotoroka.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *