Maafisa wa DCI wamkamata mshukiwa wa ulaghai

Tom Mathinji
1 Min Read
Mshukiwa wa ulaghai akamatwa na maafisa wa DCI.

Maafisa wa upelelezi wa maswala ya jinai DCI  kutoka makao makuu ya Nairobi, wamemkamata Daniel Mbugua Njogu, almaarufu Dan, nyumbani kwake mtaani Kimbo kwa madai ya ulaghai.

Njogu, mwenye umri wa miaka 30, anashtumiwa kwa kuhusika katika visa vingi vya ulaghai kupitia ubadilishanaji wa sarafu za kigeni.

Kukamatwa kwake kunajiri baada ya uchunguzi wa muda mrefu kuhusu shughuli zake ambazo zimewapotosha watu wanaowekeza katika soko la kubadilishana fedha za kigeni.

“Watu ambao wamelaghaiwa na Njogu au kupoteza fedha kupitia shughuli zake, wanahimizwa kupiga ripoti katika afisi za DCI Jijini Nairobi,” ilisema taarifa ya idara hiyo kupitia ukurasa wake wa X.

Idara ya DCI imewatahadharisha wananchi kuwa makini wanapojihusisha na biashara ya ubadilishanaji wa fedha za kigeni, au uwekezaji mwingine kupitia mtandaoni.

TAGGED:
Share This Article