Maafisa saba wa KPLC washtakiwa kwa uhalifu wa kiuchumi

Tom Mathinji
1 Min Read

Maafisa saba wa kampuni ya usambazi umeme KPLC, wamepatikana na makosa ya uhalifu wa kiuchumi, uliosababisha kampuni hiyo kupoteza shilingi milioni 150.

Kesi hiyo iliwasilishwa na afisi ya mkurugenzi wa mashtka ya umma ODPP, katika mahakama ya kusikiza kesi za ufisadi za milimani.

Maafisa hao saba wanajumuisha Harun Karisa Meneja Mkuu kitengo cha fedha, Mhandisi Dkt. Noah Ogano Omondi, mwanachama wa kamati ya kutathmini, Mhandisi Daniel Ochieng Muga. kaimu mkuu wa kitengo cha usambazaji, Mhandisi John Mwaura Njehia mwanachama wa kamati ya kutathmini zabuni, James Muriuki, mwanachama wa kamati ya kutathmini zabuni, Bernard Muturi na mhandisi Evelyne Pauline Amondi mwanachama wa kamati ya kufungua zabuni.

Kulingana na ODPP, maafisa hao wanakabiliwa na mashtaka ya kupanga kutekeleza uhalifu wa kiuchumi, kuambatana na sehemu ya 47A (3) pamoja na sehemu ya 48 ya sheria zinazokabiliana na ufisadi za mwaka 2003.

Upande huo wa mashtaka ukiongozwa na uliiambia mahakama kuwa, maafisa hao walizembea katika mchakato wa kutoa zabuni, na kusababisha kutolewa kwa zabuni licha ya kuwa na kasoro kadhaa ambapo shilingi milioni 150 zilitolewa kwa wanakandarasi.

Kesi hiyo itatajwa Oktoba 15,2024.

TAGGED:
Share This Article