Maafisa 17 wakamatwa kwa ufisadi Nyayo House

Dismas Otuke
1 Min Read

Maafisa 17 wa idara ya uhamiaji inayohusika na uchapishaji pasipoti katika jumba la Nyayo, wamekamatwa tangu kuanza kwa msako dhidi ya ufisadi unaoendeshwa na majasusi.

Waziri wa Usalama wa Kitaifa Kithure Kindiki alisema hayo jana Alhamisi alipofika mbele ya kamati ya bunge la kitaifa inayosimamia maswala ya utangamano wa kikanda.

Msako huo umekuwa ukiendeshwa katika afisi hizo kuanzia mwezi Septemba mwaka jana, kufuatia malalamishi ya wananchi kuhusu kucheleweshwa kwa uchapishaji wa pasipoti.

Waziri alikiri kuwepo kwa changamoto ya uchapishaji wa stakabadhi hizo lakini akaahidi kuzisuluhisha hivi karibuni.

Kulingana naye, uchechefu wa fedha umekuwa kikwazo kikuu na tayari serikali imelipa madeni ya shilingi bilioni 380 yaliyochangia kukwama kwa uchapishaji au kasi ya chini ya uchapishaji wa pasipoti.

Share This Article