Kundi la waasi la M23 limejitolea kuhusika katika mazungumzo ya amani nchini DRC.
Akihutubia wanahabari mjini Goma, Kanali Corneile Ngaa, kiongozi wa kundi la River Alliance linaloungwa mkono na kundi haramu la M23, walielezea haja ya pande zote kufuata mwafaka amani.
Tayari serikali ya DRC na M23 wameelezea matumaini ya kupata suluhu kupitia kuheshimu mwafaka wa amani wa Julai 19 mwaka huu.