Bingwa wa Dunia Noah Lyles ndiye bingwa mpya wa Olimpiki katika mbio za mita 100, baada ya kuziparakasa kwa sekunde 9.79 huku fedha ikitwaliwa na Kishane Thompson wa Jamaica.
Fred Kerley pia wa Marekani alijinshindia medali ya shaba katika fainali hiyo ya kukata na shoka, iliyoandaliwa ugani Stade de France Jumapili usiku.
Marekani ilinyakua dhahabu ya Olimpiki katika makala ya mwaka huu baada ya subira ya miaka 20.