Shericka Jackson wa Jamaica na Noah Lyles wa Marekani wamedhihirisha umaahiri wao baada ya kuhifadhi mataji ya dunia ya mita 200 katika siku ya saba ya mashindano yanayoendelea mjini Budapest,Hungary Ijumaa usiku.

Jackson akiyekuwa ameshinda fedha katika mita 100 mwaka huu akikamilisha fainali hiyo akiweka rekodi mpya ya mashindano ya sekunde 21 nukta 41, akifuatwa na Gabrielle Thomas wa Marekani kwa sekunde 21 nukta 81 , huku Sha Carri Richardson wa Marekani pia akinyakua nishani ya shaba kwa sekunde 21 nukta 91.

Lyles alihifadhi taji ya wanaume akiziparakasa kwa sekunde 19 nukta 52,akifuatwa na mwenzake Erriyon Khighton kwa sekunde 19 nukta 75, huku Letsile Tebogo wa Botswana akiridhia nishani ya shaba kwa sekunde 19 nukta 81.