Luis Rubiales ajiuzulu urais wa FA ya Uhispania baada ya busu

Martin Mwanje
1 Min Read

Luis Rubiales amejiuzulu nafasi ya rais wa Shirikisho la Soka la Uhispania baada ya kukosolewa kwa kumbusu mshambuliaji wa Uhispania Jenni Hermoso baada ya fainali ya Kombe la Dunia la Wanawake.

Hermoso, 33, alisema busu hilo baada ya Uhispania kuwapiga Uingereza halikuwa la maafikiano na aliwasilisha malalamiko ya kisheria Jumanne iliyopita.

Rubiales alisema katika taarifa kuwa amewasilisha kujiuzulu kwake kwa kaimu rais wa shirikisho Pedro Rocha.

“Siwezi kuendelea na kazi yangu,” alimwambia Piers Morgan kwenye kipindi chake cha televisheni.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 46 pia amejiuzulu wadhifa wake wa makamu wa rais wa kamati kuu ya Uefa.

Busu hilo limezua mzozo kwenye soka la Uhispania katika wiki za hivi karibuni na kufunika ushindi wa Uhispania wa Kombe la Dunia, huku Rubiales akipuuza wito wa mara kwa mara wa kujiuzulu.

Siku ya Ijumaa, mwendesha mashtaka aliwasilisha malalamiko katika mahakama kuu ya Uhispania, baada ya ushahidi wa Hermoso siku ya Jumanne dhidi ya Rubiales kwa unyanyasaji wa kijinsia.

Rubiales alidai busu hilo lilikuwa “la kuheshimiana na “ridhaa”

“Baada ya kusimamishwa kwa haraka na Fifa, pamoja na kesi nyingine za wazi dhidi yangu, ni dhahiri kwamba sitaweza kurejea kwenye nafasi yangu,” taarifa ya Rubiales ilisema.

Share This Article