Lori la kusafirisha mafuta ya kupika laanguka Gitaru

Tom Mathinji
1 Min Read
Lori la kusafirisha mafuta ya kupikia laanguka eneo la Gitaru. Picha/Hisani.

Shughuli za uchukuzi katika barabara kuu ya Nairobi-Nakuru zilitatizwa Ijumaa asubuhi baadaya lori lililokuwa limebaba mafuta ya kupikia kuanguka katika enelo la makutano la Gitaru.

Kufuatia ajali hiyo maafisa wa polisi na wazima moto walipelekwa katika eneo hilo, huku madereva wakitakiwa kuwa waangalifu sana kwa kuwa barabara ni telezi.

Ajali hiyo ilisababisha msongamano mkubwa wa magari katika eneo hilo,na kutatiza shughuli katika barabara ya southern bypass.

Aidha ajali hiyo inajiri mwezi mmoja tu baada ya lori lililokuwa likibeba mafuta kuelekea Uganda kutoka Mombasa, kuanguka katika eneo hilo baada ya gurudumu kupasuka.

TAGGED:
Share This Article