Bingwa mtetezi Sharon Lokedi, bingwa wa mwaka 2019 Peris Jepchirchir na bingwa Boston Marathon Hellen Obiri watajitosa katika msururu wa mwisho wa mbio kuu ulimwenguni katika makala ya mwaka huu ya New York Marathon Jumapili hii, Novemba 5.
Obiri atakuwa akiwania ushindi wa marathon ya pili katika amali yake, baada ya kushinda Boston Marathon mwezi Aprili mwaka huu.
Pia anajivunia kushinda mbio za Mew York City Half Marathon mwaka huu.
Jepchirchir atakuwa roho juu baada ya kuhifadhi taji ya dunia ya nusu marathon mwaka huu, na atakuwa akisaka ushindi wa pili tangu mwaka 2019.
Lokedi kwa upande wake atakuwa akilenga kuhifadhi taji ya mwaka jana.