Katibu katika Wizara ya Afya Mary Muthoni anasema mpango ulioboreshwa wa Linda Mama umewekwa ndani ya Mamlaka ya Afya Jamii (SHA) inayosimamia utekelezaji wa Bima Mpya ya Afya ya Jamii (SHIF).
Mpango huo husaidia kina mama wajawazito ili kuhakikisha wanapata huduma bora za matibabu kabla, wakati na baada ya kujifungua.
“Linda Mama mpaka saa hii iko pale ndani. Lakini tukaipamba kabisa, tukasema, la kwanza, mama akipata mimba, kuna sehemu ambayo unafaa kwenda, ile tunaita clinic. Inaitwa kwa Kizungu Prenatal care. Hakuna mama anafaa kungoja nyumbani mpaka aende ajifungue. Ni vizuri uende uangaliwe na Daktari, ndio uambiwe huyo mtoto wako anaendelea vizuri na pia wewe mwenyewe, ndio tupunguze the maternal deaths (vifo vya kina mama vinavyotokea wakati wakijifungua) yenye inapatikana kila mara.,” amesema Muthoni juu ya mpango huo ambao awali ulihofiwa utaondolewa kufuatia ujio wa SHA.
” Kwa hivyo hii Linda Mama, tumesema before delivery, mama aende hospitali aangaliwe, during delivery, ile ya kitambo Linda Mama ulikuwa unaambiwa wewe leta karai, kuja na wembe, uleta mpaka makasi, karibu uambiwe ulete kitanda ndio ulalie halafu ujifungue. Saa hii tunaambia wamama, wewe fanya mambo yako, ikifika ile siku, jifikishie pale hospitali,” aliongeza Katibu huyo wakati akizngumza mjini Eldoret.
Muthoni aliongeza kuwa chini ya mpango ulioboreshwa wa Linda Mama, kina mama wakijifungua, wataendelea kupata huduma za matibabu ili kushauriwa na wahudumu wa afya jinsi ya kumlinda mtoto ikiwa ni pamoja na siku ya kupata chanjo.