Kinyang’anyiro cha Ligi Kuu nchini Kenya kwa wanaume kitaingia raundi ya 14 leo kwa jumla ya mechi nne za Jumamosi na nyingine tano za Jumapili.
FC Talanta watakuwa ziarani katika uwanja wa Utalii Sports kumenyana na Nairobi City Stars kuanzia saa tisa, wakati mabingwa watetezi Gor Mahia wakiwa wageni wa Kenya Police FC, katika uchanjaa wa Sportspesa Arena kaunti ya Muranga kuanzia saa tisa.
Mara Sugar FC watakuwa nyumbani Awendo Green dhidi ya Kariobangi Sharks FC mida ya saa nane, nao Kakamega Homeboyz wacheze nyumbani MumiasSports Complex pia saa nane juu ya alama dhidi ya Ulinzi Stars.
Kesho Jumapili Tusker FC watajaribu kuweka kando masaibu ya kipigo cha AFC Leopards kati kati ya wiki,wakiwaalika Bidco United FC uwanjani Dandora kuanzia saa saba,kabla ya kuwapisha Shabana FC dhidi ya vinara Kenya Commercial Bank uwanjani Gusii.
Mathare United watakuwa Ukunda dhidi ya Bandari FC saa tisa wakati Muranga Seal ikiwa mwenyeji wa Posta Rangers pia mida ya saa tisa alasiri.
Sofapaka FC itakwangurana na AFC Leopards SC katika kiwara cha Dandora saa kumi katika mchuano wa kufunga pazia.