Ligi kuu ya Kenya itaendelea wikendi hii kwa mechi za raundi ya nne katika nyuga mbali mbali.
Bidco United wanaosaka ushindi wa kwanza watawaalika Talanta FC,nao Polisi FC wakiwa nyumbani dhidi ya AFC Leopards,Shabana FC wakishikane mashati na Kariobangi Sharks kasha Tusker FC wakamilishe ratiba nyumbani dhidi ya Muhoroni Youth .
Mechi zote zitangóa nanga saa tisa alasiri.
Jumapili Kakamega Homeboyz watakuwa wenyeji wa mabingwa watetezi Gor Mahia,KCB iwe nyumbani dhidi ya Bandari FC nao viongozi wa ligi Posta Rangers wapimane ubabe na Muranga Seal .
Rangers na Gor Mahia wamezoa pointi 7 kila moja baada ya mechi 3 wakifuatwa na Bandari Fc na muranga seal kwa alama 6 kila moja.
Nairobi City stars itakuwa na kibarua dhidi ya Nzoia Sugar huku Sofapaka wakimaliza kibarua ugenini kwa Ulinzi Stars wanaotafuta pointi ya kwanza baada ya kupoteza mechi zote tatu.