Ligi Kuu Kenya kuendelea Jumamosi kwa mikwangurano mitatu

KCB wanaongoza jedwali kwa alama 13,moja zaidi ya mabingwa watetezi Gor Mahia ingawa wahifadhi hela wamecheza mchuano mmoja zaidi wakati Ingwe wakikalia nafasi ya tatu kwa alama 9.

Dismas Otuke
1 Min Read

Ligi kuu ya Kenya itaendelea Jumamosi Novemba 7 kwa jumla ya mikwangurano mitatu ya raundi ya sita katika nyuga mbambali.

Limbukeni Mombasa United watakuwa nyumbani Mbaraki kuanzia saa nane adhuhuri dhidi ya Shabana FC.

Mabingwa wa ligi kuu ya daraja ya kwanza msimu jana Migori Youth, watakuwa Narok katika uwanja wa Ole Ntimama, kuanzia saa tisa dhidi ya Mara Sugar.

AFC Leopards watawinda ushindi wa tatu  watakapozuru uwanja wa Moi kaunti ya Embu dhidi ya 3K FC saa tisa.

KCB wanaongoza jedwali kwa alama 13,moja zaidi ya mabingwa watetezi Gor Mahia ingawa wahifadhi hela wamecheza mchuano mmoja zaidi wakati Ingwe wakikalia nafasi ya tatu kwa alama 9.

Share This Article