Hakimi, Mane na Diaz wateuliwa kuwania tuzo ya mwanasoka bora mwaka 2026

Mshindi atabainika katika hafla itakayoandaliwa jiji Lagos, Nigeria tarehe 7 mwezi ujao.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mshindi wa mwaka jana wa tuzo ya mwanasoka bora  barani Afrika (CAF) Achraf Hakimi wa Morocco na PSG, mshindi wa zamani Sadio Mane wa Senegal na Al Nasr, na Brahim Diaz wa Morocco na Real Madrid, ni miongoni mwa wanandinga kumi walioteuliwa kuwania tuzo ya mchezaji bora mwaka huu.

Wengine katika orodha hiyo ya kumi bora ni pamoja na Amad Diallo (Côte d’Ivoire/Manchester United), Yoane Wissa (DR Congo/Newcastle United), Antoine Semenyo (Ghana/Manchester City), Ismael Saibari (Morocco/Bayern Munich) na Ismaila Sarr (Senegal/Crystal Palace).

Aidha, orodha hiyo inawajumuisha Pape Gueye (Senegal/Villarreal) na Teboho Mokoena (South Africa/Mamelodi Sundowns).

Mshindi atabainika katika hafla itakayoandaliwa jijini Lagos, Nigeria tarehe 7 mwezi ujao.

Tuzo hiyo pia inajumuisha vitengo vya wachezaji bora kwa makipa, wachezaji bora miongoni mwa wanaosakata soka barani Afrika, klabu bora, timu bora na kocha bora wa mwaka.

Share This Article